Storm FM

Mbuzi mwenye jinsia 2 azua taharuki Nyantorotoro B

3 April 2026, 16:42

Mbuzi mwenye jinsia mbili ambaye aliyezua taharuki katika mtaa wa Nyantorotoro B. Picha na Ester Mabula

‘Huyu mbuzi nilipewa zawadi kule Kigoma na nilielezwa yuko vizuri tu kwani alizaa, lakini nashangaa nimefika Geita nashangaa watoto wanasema hana sehemu ya kutoa haja” – Catherine Kachwere, mmiliki wa mbuzi

Na: Ester Mabula

Catherine Kachwere mkazi wa mtaa wa Nyantorotoro B halmashauri ya manispaa ya Geita ametelekeza mbuzi wake kwa Balozi wa eneo hilo kutokana na kile alichoeleza utata wa jinsia ya mbuzi huyo.

Akizungumza na Storm FM Bi. Catherine amesema alipewa mbuzi huyo kama zawadi baada ya kumtibu mgonjwa aishiye mkoani Kigoma ambapo alivyo rejea nyumbani kwake alishangaa kuona maumbile ya mnyama huyo.

Sauti ya Catherine Kachwere, mmliki wa mbuzi
Bi. Catherine Kachwere, mmliki wa mbuzi mwenye jinsia 2 akizungumza na Storm FM. Picha na Ester Mabula

Balozi wa eneo hilo shina namba 20 mtaa wa Nyantorotoro B, Bw. Damian Mosha amethibitisha juu ya tukio hilo akieleza jinsi alivyoachiwa mbuzi huyo.

Sauti ya Balozi Damian Mosha
Bw. Damian Mosha, Balozi wa shina namba 20 mtaa wa Nyantorotoro B. Picha na Ester Mabula

Daktari wa mifugo kutoka manispaa ya Geita Jason Mutayaba amesema wanyama pia huzaliwa na jinsi mbili au wakati mwingine hukosa baadhi ya viungo vya mwili ambapo changamoto hiyo husababishwa na mifugo ukoo mmoja kujamiiana

Sauti ya Daktari wa mifugo, Jason Mutayaba