Storm FM
Storm FM
2 April 2026, 15:02

Katika hali ya kushangaza diaba lenye pombe ndani yake limekutwa likiwa na kinyesi ndani yake hali ambayo imeuzua taharuki kwa wananchi.
Na: Kale Chongela
Elizabeth Francisco, mkazi wa mtaa wa Mkoani kata ya Kalangalala, halmashauri ya manispaa ya Geita ameiomba serikali ya mtaa huo kumchukulia hatua mtu aliyedaiwa kujisaidia haja kubwa katika diaba lake lililokuwa na pombe za kienyeji.
Akizungumza na Storm FM leo Bi. Elizabeth Francisco amesema tukio hilo limemsababishia hasara kubwa kwani uuzaji wa pombe za kienyeji ndicho chanzo chake kikuu cha kipato akifafanua kuwa baada ya kubaini kinyesi katika diaba lililokuwa na pombe ameshindwa kufanya biashara.
Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamedai kusikitishwa na tukio hilo wakiomba mhusika achukuliwe hatua ili kudumisha usafi na heshima katika jamii.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa huo Bw. Salvatory Daniel Paul amekiri kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa jitihada bado zinaendelea za kumtafuta mhusika wa tukio hilo.
