Storm FM
Storm FM
27/03/2026, 19:11

Tanzania ina wagonjwa wapatao 6700 wa Himofilia ambapo mikakati mbalimbali imeendelea kuchukuliwa na serikali katika kurahisisha matibabu ya ugonjwa huo kwa urahisi.
Na: Ester Mabula
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita imezindua rasmi mradi wa mpango jumuishi wa huduma za himofilia na sikoseli Tanzania ambao utatekelezwa katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo mkoa wa Geita.
Mpango huo unajumuisha utoaji elimu kwa watoa huduma za Afya juu ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa changamoto hiyo sambamba na kuwezesha hospitali kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa/
Kaimu msaidizi wa mradi Dkt. Abdallah Makala amesema ugonjwa huo unasababishwa na damu kukosa uwezo wa kuganda ambapo inaelezwa kuwa katika kila watu elfu 10 Duniani kote mtu mmoja miongoni mwao ana ugonjwa huo ambapo nchini Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa 6,700.
Mgeni rasmi Mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dkt. Omari Sukari amesema jitihada za serikali ni kuhakikisha wagonjwa wa himofilia wanapata huduma za kimatibabu ambapo amehimiza watoa huduma kuendelea kutoa elimu ili wananchi wapate uelewa juu ya ugonjwa huo.

Baadhi ya wagonjwa wenye changamoto hiyo akiwemo Abdallah Muhana na Devotha Crispin ambaye ni mzazi wa mtoto mwenye ugonjwa huo wameeleza changamoto wanazopitia kutokana na ugonjwa huo
Uzinduzi wa mradi huo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita utawezesha matibabu kupatikana kwa urahisi kwa wagonjwa ambapo wataalamu wa afya wapatao 1600 wamepatiwa mafunzo ya kutibu wagonjwa hao
