Storm FM

Maafisa usafirishaji Geita waendelea kunufaika kupitia BCRO

26/02/2026, 13:51

Mgeni rasmi, Diwani wa kata ya Kalangalala akizungumza na wanachama wa BCRO (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

“Ndani ya miaka yangu mitano nitaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali na watu wote wa kata ya Kalangalala ikiwemo na nyie maafisa usafirishaji ili muweze kujikwamua kiuchumi” – Reuben Sagayika

Na: Ester Mabula

Asasi ya BCRO (Bajaj In Community Reform Organization) imeendelea kuwezesha maafisa usafirishaji wa bajaj katika mikoa mbalimbali nchini kwa kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili kupata mikopo ya bajaj itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

Jana Februari 25, 2026 vijana watatu mkoani Geita wamekabidhiwa bajaj kupitia mpango huo, ambapo mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kalangalala, ameipongeza asasi ya  BCRO na kuahidi ataendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi kwa maafisa usafirishaji kwa kuwasogeza karibu na wataalam mbalimbali ili kupata elimu hususani ya mikopo.

Sauti ya mgeni rasmi, Reuben Sagayika

Kwa upande wake, Meneja wa tawi la benki ya FINCA mkoa wa Geita ameeleza kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na BCRO ili kutoa mikopo nafuu kwa vijana.

Sauti ya meneja wa FINCA Geita Julius Matemu
Bajaj zilizotolewa na kukabidhiwa kwa wanachama watatu wa BCRO Geita. Picha na Ester Mabula

Baadhi ya wanachama pamoja na mwenyekiti wa BCRO mkoa wa Geita wameipongeza asasi hiyo kwa jitihada zake za kuwaunganisha na taasisi za kifedha, wakisema hatua hiyo imekuwa chachu ya mabadiliko ya maisha yao na familia zao.

Sauti ya wanachama wa BCRO Geita

Hata hivyo Diwani Sagayika ameahidi kuwasaidia fedha kiasi cha shilingi laki tano kwaajili ya ununuzi wa viti vya ofisi ya BCRO Geita sambamba na kuahidi kufanyia kazi changamoto ya kompyuta kupitia taarifa waliyowasilisha awali.

Mgeni rasmi Reuben Sagayika akiwa na baadhi ya wanachama wa BCRO baada ya kukabidhi Bajaj. Pichana na Ester Mabula