Storm FM

Watumishi 209 (Ajira mpya) Manispaa ya Geita wapigwa msasa

25 February 2026, 12:15 pm

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Geita Yefred Myenzi akihitimisha mafunzo. Picha na Ester Mabula

“Naamini baada ya mafunzo haya mtaendelea kuwa na utendaji wenye tija na kuzingatia miiko ya utumishi wa UMMA kwa kujiepusha na vitendo vyenye kujenga taswira mbaya ya Serikali kwenye Jamii” -Mkurugenzi Yefred Myenzi

Na: Ester Mabula

Jumla ya watumishi 209 kutoka kada mbalimbali ambao ni waajiriwa wapya halmashauri ya manispaa ya Geita wamepewa mafunzo ya siku 2 yaliyofanyika Februari 23 – 24, 2026 ambayo yalilenga kuwajengea uwezo kwa kuwapatia maarifa na ujuzi utakaowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.

Akihitimisha mafunzo hayo jana Februari 24, 2026, Mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenzi amewaasa watumishi hao kuzingatia miiko ya utumishi na kuachana na vitendo vyenye kujenga taswira mbaya ya Serikali kwenye Jamii.

Sauti ya mkurugenzi wa manispaa, Yefred Myenzi
Baadhi ya watumishi wa kada mbalimbali waliopatiwa mafunzo ya kuboresha utendaji kazi. Picha na Ester Mabula

Kaimu mkuu wa idara ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu Manispaa ya Geita Kadole Ngumungu, ametaja kada mbalimbali zilizopatiwa mafunzo sambamba na kutaja maeneo mahsusi yaliyofundishwa huku akieleza dhamira ya mafunzo hayo

Sauti ya kaimu mkuu wa idara, Kadole Ngumungu
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Geita Said Lupunjaje akizungumza baada ya kuhitimisha mafunzo. Picha na Ester Mabula

Akizungumza mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Geita Said Lupunjaje aliyetoa mafunzo kwa watumishi hao amesema Taasisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa watu mbalimbali huku baadhi ya watumishi waliopewa mafunzo wakipongeza uwepo wa mafunzo hayo na kueleza namna watakavyo yatumia katika utendaji wao wa kazi.

Sauti ya mkuu wa TAKUKURU na watumishi
Baadhi ya watumishi (ajira mpya) wa kada mbalimbali waliopatiwa mafunzo. Picha na Ester Mabula