Storm FM
Storm FM
18 February 2026, 1:28 pm

Chama cha ushirika kimekuwa na fursa mbalimbali ya kuwaunganisha wakulima katika kujadili na kufanya mambo ya kuleta tija kwenye kilimo.
Na: Kale Chongela
Chama cha ushirika cha Lwamgasa Farmers Amocos Limited kilichopo wilaya ya Geita mkoani Geita kimefanya harambe kwa ajili ya kuchangisha fedha ili kununua trekta na vifaa vya kilimo.
Diwani wa kata ya Lwamgasa Bw. Daniel Mabala akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye alitarajiwa kuwa Naibu waziri TAMISEMI ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia afya Dkt. Jafari Rajabu Seif, amewapongeza wakulima kwa kuendelea kuonesha ushirikiano na kuhakikisha kila mkulima analima kilimo cha kisasa.
Mwenyekiti wa Chama hicho cha ushirika Bw. Abdallah Rajabu ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayongoza na Dkt. Samia Suluhu kwa kutoa fedha ili kufanikisha upatikanaji wa mbegu na mbolea.

Meneja wa chama hicho cha Ushirika Ndugu Msafiri Makoye amesema chama hicho kimekuwa na mchango mkubwa kwa wakulimu huku akiwasihi wakulima wengine kujiunga na chama hicho.
