Storm FM
Storm FM
17 January 2026, 2:07 pm

“Jumla ya watuhumiwa 200 tumewakamata kwa makosa mbalimbali na tunaendelea na upelelezi zaidi ili kuwafikisha mahakamani” – SACP Safia Jongo
Na: Ester Mabula
Jeshi la polisi mkoa wa Geita limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa kupitia oparesheni mbalimbali ambapo kwa kipindi cha kuanzia Januari mosi, 2026 hadi leo Januari 17, 2026 limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 200 wa makosa mbalimbali.
Hayo yameelezwa leo Januari 17, 2026 na Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Safia Jongo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ameesema miongoni mwa wathumiwa waliokamatwa mtuhumiwa mmoja amekamatwa akiwa na mtambo wa kuchapisha noti bandia.

