Storm FM

Felista adaiwa kuiba nguo za ndani za jirani yake Geita

15 January 2026, 2:59 pm

Picha hii siyo uhalisia ni kutoka mtandaoni

Mmiliki wa nguo hizo licha ya kukiri kuwepo kwa ugonvi kati yake na jirani yake amesema kiu yake ni kupata nguo zake.

Na Kale Chongela:

Felista Tablei mkazi wa mtaa wa Mkoani Kata ya Kalangalala Manispaa ya Geita amefikishwa ofisi ya serikali ya mtaa huo kwa tuhuma za kuiba nguo za ndani nakuchana shuka la jirani yake.

Wahenga walisema kua uyaone , Bi Felista amejikuta chini ya ulinzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa mkoani Manispaa ya Geita kwa tuhuma za kuiba nguo za ndani nakuchana shuka.

Tumezungumza na Felista kutaka kufahamu undani wa tukio hilo ambapo amekiri kuchukua nguo ya ndani moja na dela la jirani yake kutokana na ugonvi wao uliochangiwa na dada wa kazi aliyekuwa akifanya kazi kwa jirani yake kisha kuhamia kwake.

Sauti ya Felista Mtuhumiwa

Kwa upande wake Odetha Dickson mmiliki wa nguo hizo licha ya kukiri kuwepo kwa ugonvi kati yake na jirani yake amesema kiu yake ni kupata nguo zake huku akiomba ofisi ya mtaa huo kumchukulia hatua ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Sauti ya Odetha Mlalamikaji

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mkoani Salvatory Daniely amekiri kupokea malalamiko hayo nakwamba mtuhumiwa amekiri kuchukua nguo hizo kwasababu ya hasira ya ugonvi wao huku akipigwa faini ya shilingi 75 kulipia gharama za nguo hizo.

Sauti ya Mwenyekiti Mkoani