Storm FM
Storm FM
9 January 2026, 12:11 pm

“Kimsingi zoezi la kuandikisha wanafunzi linaendelea hadi Marchi 31, 2026 kwa mujibu wa mwongozo wa serikali kupitia wizara ya elimu” – Mwalimu Mtweve
Na: Ester Mabula
Afisa elimu mkoa wa Geita Mwalimu Antony Mtweve amewahimiza wazazi na walezi kuendelea kujitokeza kwaajili ya kuandikisha wanafunzi wa awali na darasa la kwanza kwaajili wa muhula mpya wa masomo unaotarajia kuanza Januari 13, 2025.
Akizungumza leo Januari 09, 2025 akiwa katika kipindi cha Storm Asubuhi cha redio Storm FM amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale kwa kuandikisha watoto 5479 sawa na asilimia 74 kwa darasa la awali na wanafunzi 6585 sawa na asilimia 88.
Aidha Afisa elimu amebainisha kuwa nyaraka muhimu ambayo mzazi anatakiwa kuwa nayo wakati wa zoezi la kumuandikisha mtoto ni cheti cha kuzaliwa ili kuo ndoa changamoto ya majina kukosewa.