Storm FM
Storm FM
5 January 2026, 3:42 pm

“Ibada njema ni yenye kukumbuka watu wenye uhitaji na kuweza kuwasaidia ili waweze kujisikia vizuri kama watu wengine” – Diwani Sagayika
Na: Ester Mabula
Diwani wa kata ya Kalangalala Mhe. Ruben Emmanuel Sagayika ameuanza vyema mwaka 2026 kwa kuwakumbuka wagonjwa, watoto yatima pamoja na wafungwa waliopo katika gereza la wilaya ya Geita kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali.
Mahitaji hayo yalitolewa Disemba 31, 2025 ambapo akiwa katika hospitali ya halmashauri ya manispaa ya Geita ameeleza kuwa mbali na kuwagusa wagonjwa ataendelea kuwa mwakilishi wa kusemea changamoto mbalimbali ndani ya kata yake.
Watumishi katika hospitali hiyo akiwemo mganga mfawidhi Dkt. Thomas Mafuru pamoja na baadhi ya wagonjwa wamemshukuru Diwani kwa kuweza kuwapatia kwa msaada huo.

Akiwa katika gereza la wilaya ya Geita amesema serikali ya awamu ya sita inatambua makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii huku Mkuu wa Gereza la Geita Mrakibu wa polisi Jovin Bugwina akitoa wito kwa wadau wengine kufata nyayo za kiongozi huy
Katika hatua nyingine diwani Sagayika ametoa zawadi kwa watoto Yatima wanaolelewa katika kituo Cha moyo wa huruma ambapo msimamizi mkuu wa kituo hicho Sister Maria Lauda amemshukuru diwani kwa kuongeza tabasamu katika nyuso za watoto hao huku akiikumbusha Jamii kuendelea kuwasaidia kwani mahitaji ya watoto ni mengi.
