Storm FM
Storm FM
4 December 2025, 6:28 pm

Ikiwa ni siku chache tangu kuapishwa rasmi kwa madiwani wateule watakaoongoza kuanzia 2025 hadi 2030, sasa wameanza rasmi majukumu.
Na: Ester Mabula
Diwani mpya wa Kata ya Kalangalala, Reuben Emmanuel Sagayika, amekabidhiwa rasmi ofisi leo Disemba 04, 2025 kutoka kwa mtangulizi wake, Mhe. Prudence Temba, katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kata hiyo.
Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, watendaji wa mitaa na kata, wenyeviti wa mitaa ya kata hiyo pamoja na wakuu wa idara katika ngazi ya kata ikiwemo afya na elimu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi, Diwani Sagayika aameahidi kushirikiana na viongozi wa kata hiyo ambapo ameahidi kutembelea mitaa yote 11 iliyopo katika kata kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi

Kwa upande wake, Diwani aiyemaliza muda wake Mhe. Prudence Temba amempongeza mrithi wake na kumtakia utendaji uliojaa maadili huku akiahidi kushirikiana naye wakati wowote atakaohitajika.
