Storm FM
Storm FM
27 November 2025, 4:28 pm

Msako wa vijana ambao wanakaa kwenye vijiwe vya Bodaboda bila kazi kuanza Manispaa ya Geita Mkoani Geita
Na Kale Chongela:
Umoja wa waendesha Bodaboda Mkoa wa Geita umepiga marufuku baadhi ya waendesha pikipiki ambao kwasasa hawana vyombo hivyo kukaa kwenye maegesho bila kazi yoyote ya kufanya.
Katazo hilo limetolewa na Katibu msaidizi wa umoja huo George Manyogote ambapo amesema vijana kukaa kwenye vijiwe vya bodaboda bila vyombo hivyo haikubaliki kwani wengi wao wameanza kujihusisha na vitendo vya uchezaji wa kamali ishara ambayo siyo nzuri siku za usoni.

Mwenyekiti wa Egesho la waendesha Bodaboda Mtaa wa Lukilini Kata ya Kalangalala Manispaa ya Geita Bw Dausoni Christopha amekiri uwepo wa vijana ambao hawapo awali walikuwa na vyombo hivyo lakini kwasasa hawana na wanashinda vijiweni.
Watumiaji wa usafiri huo na baadhi ya waendesha pikipiki Manispaa ya Geita wamepongeza hatua hiyo yenye lengo la kukabiliana na vitendo vya uhali vinavyoweza kusababishwa na hali hiyo.
Storm FM inaendelea na jitihada za kuwatafuta vijana hao wanaodaiwa kukaa vijiweni bila pikipiki ili hali walikuwa na vyombo hivyo ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo nakuzifikisha kwa mamlaka husika ili zipatiwe ufumbuzi.