Storm FM
Storm FM
18 November 2025, 12:02 pm

Jeshi la polisi limewataka waendesha Bodaboda mkoani Geita kuepukana na matukio yanayoweza kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Na Edga Rwenduru:
Jeshi la polisi mkoani Geita limetoa maelekezo kwa umoja wa waendesha pikipiki mkoa wa Geita kuhakikisha wanasimamia sheria ndogo ndogo walizojiwekea kwenye maegesho yao kwa lengo la kuwadhibiti boda boda wanaokiuka kwa makusudi sheria za usalama barabarani.
Maelekezo hayo ya metolewa na Mkuu wa oparesheni wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa polisi ACP Amon Mimata katika kikao kati ya jeshi la polisi na waendesha pikipiki maarufu kama Boda boda chenye lengo la kuzungumzia usalama, kuelekea mwisho wa mwaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha waendesha Pikipiki mkoa wa Geita Fred Fidel amewaagiza wenyeviti wa Bodaboda wilaya zote za mkoa wa Geita kuhakikisha wanasimamia ipasavyo sheria hizo walizojiwekea kwenye maegesho yao na atakaekiuka sheria hizo achukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwenye egesho.

Nao baadhi ya Viongozi wa maegesho wameahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa na jeshi la polisi ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza.
Hata hivyo Jeshi la polisi limewataka waendesha Bodaboda mkoani Geita kuepukana na matukio yanayoweza kuhatarisha usalama wa maisha yao na amani ya nchi kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara kama yaliyotokea katika vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi.