Storm FM
Storm FM
27 October 2025, 11:41 am

Oktoba 29, 2025 ni siku ambayo Taifa la Tanzania litafanya uchaguzi mkuu wa kuchagua wabunge, madiwani na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Na: Ester Mabula
Mgombea udiwani (CCM) kata ya Kalangalala Reuben Sagayika amewahimiza wananchi wa kata ya Kalangalala na watanzania kwa ujumla kujitokeza kuweza kupiga kura ya kuchagua viongozi wa CCM kwa nafasi za udiwani, ubunge na Rais ili walete maendeleo.
Akizungumza leo Oktoba 27, 2025 wakati akifanya mahojiano na redio Storm FM amesema yapo mengi yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho katika awamu zilizopita na kwamba wananchi wawachague ili kuendeleza yale mazuri ya maendeleo yaliyoanzishwa.
Katika hatua nyingine ameeleza kuwa yuko tayari kuwatumikia wananchi wa kata ya Kalangalala kwa rika zote bila kuwa na ubaguzi akiamini katika uongozi wa uwazi na maendeleo kwa watu wote.
Tume huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) ilitangaza rasmi kuwa siku ya uchaguzi mkuu nchini itakuwa Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ambapo tarehe hiyo imetangazwa kuwa siku ya mapumziko ili wananchi washiriki katika zoezi la kupiga kura.