Storm FM

CCM yatoa elimu ya kupiga kura kwa vitendo jimbo la Geita

21 October 2025, 10:06 pm

Mratibu wa kampeni Jimbo la Geita akitoa elimu kwa vitendo ya kupiga kura. Picha na Mrisho Sadick

Elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu mchakato wa upigaji kura, ili kuhakikisha kila kura inayopigwa inahesabiwa ipasavyo.

Na Mrisho Sadick:

Zikiwa zimesalia siku nane kuelekea Uchaguzi Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita kimeendelea kutoa elimu kwa vitendo kwa wanachama wake na wananchi kuhusu namna sahihi ya kupiga kura, ili kuepuka kura kuharibika na kushindwa kuhesabiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo katika kata tatu za Jimbo la Geita, Mratibu wa Kampeni wa jimbo hilo ambaye pia ni Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Geita, Bi Joyce Ong’eng’o amewataka wanachama na wananchi kuhakikisha wanafuata utaratibu uliowekwa wakati wa kupiga kura.

Mratibu wa kampeni Jimbo la Geita akitoa elimu kwa vitendo ya kupiga kura. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya wanachama na wananchi waliopata elimu hiyo wamesema imewasaidia kuelewa vizuri taratibu za kupiga kura, jambo litakalowasaidia kushiriki ipasavyo katika uchaguzi ujao bila makosa.

Mratibu wa kampeni Jimbo la Geita akizungumza na wanachama wa CCM Lwezera. Picha na Mrisho Sadick