Storm FM

Mradi wa maji miji 28 upo hatua za mwisho Geita

20 October 2025, 11:50 am

Sehemu ya miundombinu ya mradi wa miji 28 katika kijiji cha Senga Geita DC. Picha na Mrisho Sadick

Mradi wa Maji wa Miji 28 Geita ni sehemu ya mpango wa kitaifa unaotekelezwa katika mikoa kadhaa ikiwemo Geita

Na Mrisho Sadick:

Serikali Mkoani Geita imemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa miji 28 wa Bilioni 124 kuhakikisha anakamilisha mradi huo ndani ya siku 60 zilizobaki kwa mujibu wa mkataba.

Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa na Kamati ya usalama ya mkoa huo ametembelea nakukagua katika chanzo cha mradi huo unaotoa maji ziwa Victoria katika Kijiji Cha Senga Halmashauri ya wilaya ya Geita nakutoa maagizo kwa mkandarasi huku mkuu wa wilaya ya Geita Hashim akimshukuru Rais Dkt Samia kwa kutoa fedha za mradio nakwamba yeye pamoja na viongozi wenzake watausimamia hadi pale mkandarasi atakapomaliza utekelezaji.

Mkuu wa mkoa wa Geita akiwa katika ukaguzi wa mradi wa miji 28 katika kijiji cha Senga. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Geita

Awali mkurugenzi mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiraa mjini Geita GEUWASA Mhandis Frank Changawa amesema mwishoni mwa mwezi disemba mradi huo utakuwa umekamilika nakwamba utawanufaisha watu zaidi ya 360,000 Kutoka Kata 13 za Manispaa ya Geita na vijiji 19 Kutoka Geita DC.

Sauti ya Mkurugenzi GEUWASA
Baadhi ya mafundi wakiendelea ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Senga. Picha na Mrisho Sadick

Wakazi wa Kata ya Senga, ambako ndipo chanzo cha mradi kipo, wameahidi kulinda miundombinu ya maji hiyo kwa manufaa ya wananchi wote wa Mkoa wa Geita na kusaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu.

Sauti ya Wananchi Senga

Mradi wa Maji wa Miji 28 Geita ni sehemu ya mpango wa kitaifa unaotekelezwa katika mikoa kadhaa ikiwemo Geita kwa lengo la kuhakikisha maji ya Ziwa Victoria yanawanufaisha wakazi wengi zaidi nchini.