Storm FM
Storm FM
18 October 2025, 3:52 am

Ni mchaka mchaka kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu, ambapo mgombea wa Ubunge Jimbo la Busanda kwa tiketi ya CCM ameendelea kusaka kura kwa wananchi.
Na: Ester Mabula
Mgombea Ubunge wa jimbo la Busanda kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif, amewaomba wanachama na wananchi wa kijiji cha Ndelema, kata ya Kamena kujitokeza kwa wingi na kuichagua CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.
Akizungumza Oktoba 17, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika tawi la CCM Ndelema, Dkt. Jafari amesisitiza kuwa ajenda ya kuanzishwa kwa halmashauri mpya ni moja ya kipaumbele chake kikuu atakachokibeba kwa nguvu zote endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Busanda.

Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa CCM itaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi wa Busanda, huku akitoa wito kwa wakazi wa Ndelema kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.

