Storm FM
Storm FM
14 October 2025, 11:19 am

“Vilevile tunaendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kwa kushirikiana na serikali ikiwemo sekta za Afya na elimu” – Katibu wa tawi la Simba Mpomvu
Na: Edga Rwenduru
Mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba katika mtaa wa Mpomvu uliopo kata ya Mtakuja halmashauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita wametumia kiasi cha shilingi milioni tatu kukamilisha ujenzi wa mnara wa kisasa katika tawi la klabu hiyo ambao umejengwa eneo la barabarani Mpomvu.
Akizungumza na Storm FM, mwenyekiti wa tawi hilo Bw.Yohane Mathias amesema tawi hilo lina zaidi ya wanachama 50 ambao wanakidhi vigezo huku wakiwa na nia ya kuendelea kuvuna wanachama wengi zaidi.
Aidha viongozi wa tawi hilo akiwemo Katibu wa tawi Masolwa Yombo wamesema tawi hilo pia linashiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama kusaidia kwenye ujenzi wa zahanati na shule katika mtaa huo pamoja na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyio waliyojitokeza katika uzinduzi wa mnara huo wamepongeza hatua hiyo na kueleza pia kufurahishwa na usajili wa klabu hiyo kwa msimu huu unaoendelea huku wakitarajia matokeo mazuri zaidi.
