Storm FM
Storm FM
10 October 2025, 6:51 am

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufika mkoani Geita Oktoba 13, 2025 ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za chama hicho.
Na: Ester Mabula
Umoja wa vijana wilaya ya Geita umeongoza mbio za picha ya mgombea urais wa chama hicho kwa lengo la kuwatangazia wananchi wa Geita juu ya ujio wa mgombea huyo wa Urais.
Akizungumza mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Geita Bi. Naomi Fujo amesema mbio hizo zitafanywa na maafisa usafirishaji ambao ni madereva boda boda pamoja na bajaji zitapita katika maeneo mbalimbali ili kuwaeleza wananchi juu ya ujio wa kiongozi wao wa chama.

Mwenyekiti wa umoja wa madereva bodaboda mkoa wa Geita Fred Fidel amesema kuwa wako tayari kuongoza mbio hizo huku akipongeza jitihada zilizofanywa na mgombea huyo katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mbio hizo ambaye pia ni mgombea ubunge (CCM) wa jimbo la Geita mjini mhandisi Chacha Wambura amepongeza hatua hiyo na kuwasihi maafisa hao wa usafirishaji kuhakikisha wanafikisha ujumbe kama ilivyo kusudiwa.
