Storm FM
Storm FM
9 October 2025, 5:34 am

Ikiwa zimesalia siku 19 tu kuweza kufanyika uchaguzi mkuu kwa mwaka 2025, wagombea wa nafasi mbalimbali wameendelea kunadi sera pamoja na ilani za vyama vyao.
Na: Ester Mabula
Mgombea udiwani katika kata ya Mtakuja kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Meya mstaafu wa manispaa ya Geita Mhe. Costantine Morandi Oktoba 08, 2025 ameendeleza kampeni za kunadi sera zake na ilani ya chama chake sambamba na kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua tena katika nafasi hiyo kwa awamu nyingine.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika eneo la Samina Senta katika kata hiyo ameeleza vipaumbele vyake kuwa ni sekta za maji, elimu sambamba na miundombinu hususani nishati ya umeme huku akitaja miradi ambayo ametekeleza kwa awamu inayokamilika chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amewasihi wananchi kuchagua viongozi wa CCM ili waweze kukamilisha malengo na mipango mizuri waliyoanzisha kwenye sekta mbalimbali huku lengo kubwa likiwa ni kuchochea maendeleo.

