Storm FM
Storm FM
8 October 2025, 5:28 am

“Suala hili tumekuwa tukilikomesha lakini inaonekana bado linajirudia kutokana na baadhi ya mawakala kuendelea kukiuka taratibu” – Mwenyekiti wa stendi Nyankumbu
Na: Kale Chongela
Baadhi ya wamiliki wa magari ya abiria katika kituo kidogo cha magari ya abiria kilichopo kata ya Nyankumbu, halmashauri ya manispaa ya Geita wamewalalamikia baadhi ya mawakala wanaotafuta abiria na kuwaelekeza kupanda magari binafisi ili hali magari hayo hayana leseni ya usafirishaji wa abiria.
Akizungumza na Storm FM jana Oktoba 07, 2025 kwa niaba ya wamiliki wa magari ya abiria Shigogo Wiliam amesema jambo hilo linawakwamisha kwani wao hulipia leseni ya usafirishji wa abiria na kwamba jambo hilo linatakiwa kutatuliwa.
Baadhi ya mawakala ambao wamekuwa wakijihusisha na tabia hiyo ya kutafuta abiria na kuwaelekeza kupanda gari binafisi wamepata nafasi ya kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.

Mwenyekiti wa stendi hiyo ya Nyankumbu Bw. Aloyce Kavula baada ya kupokea tuhuma hizo amesema amekuwa akijaribu kuzuia changamoto hiyo na kutoa adhabu kwa mawakala wanaokiuka lakini tabia hiyo imeendelea kujirudia.
Mwenyekiti wa umoja wa madereva wa magari ya abiria wa mkoa wa Geita amesema tabia hiyo inatakiwa kukoma mara moja na kwamba viongozi wa stendi wanatakiwa kuwajibika mara moja ilikukomesha changamoto hiyo
