Storm FM

Stanbic benki mkombozi kwa wachimbaji Geita

26 September 2025, 10:11 pm

Meneja wa Stanbic Bank akizunguzia huduma za benki hiyo. Picha na Mrisho Sadick

Mikopo hiyo inawahusu pia watoa huduma kwenye migodi ya dhahabu, wauzaji wa vito vya thamani pamoja na wafanyabiashara wa kada mbalimbali.

Na Mrisho Sadick:

Stanbic Bank imeendelea kuunga mkono maendeleo ya sekta ya madini nchini kwa kutoa mikopo maalum kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza tija na thamani katika shughuli za uchimbaji.

Meneja wa benki hiyo tawi la Geita Hilda Augustino akizungumza na waandishi wa Habari katika viwanja vya maonesho ya nane ya madini Mkoani Geita amesema mikopo hiyo inahusisha vifaa vya uchimbaji na mitambo mikubwa, ambapo mikopo yenyewe inajisimamia kama dhamana na inalindwa na bima maalum.

Watumishi wa Benk ya Stanbic wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Mrisho Sadick

Pamoja na wachimbaji, mikopo hiyo inawahusu pia watoa huduma kwenye migodi ya dhahabu, wauzaji wa vito vya thamani pamoja na wafanyabiashara wa kada mbalimbali na wajasiriamali.

Banda la Stanbic lililopo katika maonesho ya nane ya madini Geita. Picha na Mrisho Sadick

Wananchi na wadau wa sekta ya madini wametakiwa kutembelea banda la Stanbic Bank katika Maonesho ya Nane ya Madini ya Dhahabu yanayoendelea kwenye viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Manispaa ya Geita, ili kunufaika na huduma hizo.

Sauti ya Meneja Stanbic tawi la Geita