Storm FM
Storm FM
25 September 2025, 3:53 am

Mgombea udiwani kata ya Bukoli (CCM) Faraji Seif amewaomba wananchi wa kata hiyo kuendeleza imani na Chama cha mapinduzi kwa kuweza kuwachagua katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Na: Ester Mabula
Mgombea wa udiwani kata ya Bukoli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Faraji Rajabu Seif mapema Septemba 24, 2025 ameendesha zoezi la kuomba kura kwa kutembelea nyumba kwa nyumba katika tawi la Ikina.
Akiwa ameambatana na mabalozi wa nyumba kumi, Faraji amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 na kuwapigia kura wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu.

Zoezi hilo ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za chama hicho, likiwa na lengo la kusambaza ujumbe wa mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
