Storm FM

Mapung’o aahidi kuipeleka kata ya Butobela kileleni

24 September 2025, 9:45 am

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita (kati), Mgombea ubunge jimbo la Busanda (kushoto) na mgombea udiwani kata ya Butobela (kulia) katika picha ya pamoja. Picha na mwandishi wetu.

Vyama mbalimbali vya siasa nchini Tanzania vimeendelea kunadi sera na ilani za vyama vyao ikiwa ni kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025.

Na: Ester Mabula

Mgombea udiwani wa kata ya Butobela, jimbo la Busanda, wilaya ya Geita, Pascal Mapung’o ameahidi kushughulikia changamoto zote zinazowakabili wananchi wa kata hiyo na kuifanya Butobela kuwa sehemu salama na ya maendeleo.

Mapung’o ametoa ahadi hiyo jana Septemba 23, 2025 katika uzinduzi wa kampeni zake za udiwani uliofanyika katika uwanja wa Nyakagwe, kijiji cha Nyakagwe, ambapo amewahakikishia wananchi, viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kuwa hawatajutia kumpa kura.

Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni kata ya Butobela. Picha na mwandishi wetu

Amesema endapo atachaguliwa kuwa diwani, atahakikisha miundombinu ya barabara inaboreshwa, akitaja barabara ya Kakola–Nyakagwe hadi Bukoli kuwa moja ya kipaumbele chake kutokana na umuhimu wake katika kukuza uchumi wa wakazi wa eneo hilo.

Sauti ya Pascal Mapung’o mgombea udiwani (CCM) kata ya Butobela
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni kata ya Butobela. Picha na mwandishi wetu