Storm FM
Storm FM
21 September 2025, 8:13 am

Equity Benki imejipanga kuhakikisha wananchi wa Geita hususani wachimbaji wadogo na wakati wa madini ya dhahabu wananufaika na huduma rafiki .
Na Mrisho Sadick:
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, ameutaka uongozi wa Equity Bank kuhakikisha unaleta ubunifu mpya katika utoaji wa huduma za kifedha kwa wananchi, hususan wakulima, wafugaji na wachimbaji wa madini ya dhahabu.
Shigela ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la Equity Bank Septemba 20,2025 katika Manispaa ya Geita ambapo amesisitiza umuhimu wa taasisi hiyo kuja na huduma tofauti na zile zinazotolewa na taasisi nyingine za kifedha zilizopo mkoani humo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania Bi Isabella Maganga amesema benki hiyo imejipanga kuhakikisha wananchi wa Geita wananufaika na huduma rafiki zitakazowawezesha kupata mitaji, mikopo nafuu na elimu ya kifedha.

Wakizungumza baada ya uzinduzi huo baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Geita akiwemo Atanas Inyasi Leonard Bugomola na Richard Raphael wamepongeza hatua hiyo ya Equity Bank, wamesema itasaidia kukuza biashara na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mkoa huo.