Storm FM

CHAUMMA yaahidi kujenga viwanda Geita

16 September 2025, 8:34 pm

Wakazi wa mkoa wa Geita wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa CHAUMMA Nyankumbu. Picha na Mrisho Sadick

Mpango huo ni nyenzo ya maendeleo endelevu na njia ya kuinua maisha ya wananchi wa Geita na maeneo jirani.

Na Mrisho Sadick:

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ukombozi wa umma CHAUMMA Salum Mwalimu ameahidi kuanzisha viwanda vya ngozi na pamba mkoani Geita kama mkakati wa kuongeza thamani ya mifugo na mazao ya wakulima.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni Kata ya Nyankumbu Manispaa ya Geita Mwalimu amesema mkoa huo una fursa nyingi kutokana na wingi wa mifugo na kilimo cha pamba, hivyo ni wakati wa kuyatumia mazao hayo kuzalisha bidhaa zitakazoongeza kipato cha wananchi.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ukombozi wa umma CHAUMMA Salum Mwalimu akizungumza na wakazi wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Mkurugenzi wa kurugenzi ya Habari na taarifa kwa umma wa CHAUMMA Jonh Mrema amesema Mkoa wa Geita una ngo’mbe zaidi ya milioni moja nakwamba mpango huo ni nyenzo ya maendeleo endelevu na njia ya kuinua maisha ya wananchi wa Geita na maeneo jirani.

Mkurugenzi wa kurugenzi ya Habari na taarifa kwa umma wa CHAUMMA Jonh Mrema akiwa kwenye mkutano wa Kampeni Geita. Picha na Mrisho Sadick

Wakazi wa Manispaa ya Geita wamekuomba chama hicho kuhakikisha ahadi hizo zinatekelezwa kwakuwa  zitaleta mabadiliko makubwa kiuchumi na kijamii kwa wananchi.

Ripoti kamili na Mrisho Sadick