Storm FM

Katibu wa vijana CHADEMA Nyarugusu ajiunga CCM

13 September 2025, 2:22 pm

Mgombea ubunge (CCM) jimbo la Busanda akimkabidhi kadi ya uanachama aliyekuwa katibu wa vijana (BAVICHA) Nyarugusu. Picha na mwandishi wetu.

Vyama mbalimbali vya siasa nchini vimeendelea na kampeni ya kunadi sera za ila i ya vyama vyao kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Na: Mwandishi wetu

Aliyekuwa Katibu wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) kata ya Nyarugusu, Swaumu Musa, ametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kukabidhi kadi yake kwa Mwenyekiti wa CCM kata ya Nyarugusu.

Swaumu ameeleza kuwa amevutiwa na sera za CCM ambazo, kwa mujibu wake, ni za kueleweka na zinazotekelezeka, tofauti na zile za upinzani.

Mgombea ubunge (CCM) jimbo la Busanda Jafari Rajabu akionesha kadi za CHADEMA baada ya kumkabidhi kadi ya CCM.

Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika wakati wa kikao cha maandalizi ya kampeni za uchaguzi kilichoongozwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda kwa tiketi ya CCM, Dkt. Jafari Rajabu Seif. Kikao hicho kilifanyika katika kata ya Nyarugusu, na kililenga maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni unaotarajiwa kufanyika Oktoba 15, 2025.

Katika kikao hicho, Dkt. Jafari aliwasilisha muhtasari wa sera na mikakati yake, akieleza mambo atakayoyatekeleza endapo atapewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

Baadhi ya wananchama wa CCM waliohudhuria kikao cha maandilizi ya kampeni Jimbo la Busanda. Picha na mwandishi wetu.