Storm FM

Mradi wa mabanda ya kudumu viwanja vya maonesho Geita waendelea

5 September 2025, 10:50 am

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela akizungumza na wanahabari. Picha na Edga Rwenduru

Ikumbukwe mkoa wa Geita umekuwa ukifanya maonesho ya teknolojia ya madini kila mwaka ambapo kwa mwaka huu 2025 yatafanyika kwa mara ya 8.

Na: Edga Rwenduru

Serikali mkoani Geita imeanza ujenzi wa mabanda ya kudumu katika viwanja vya maonesho ya Dkt. Samia Suluhu Hassan zamani EPZA vilivyopo kata ya Bombambili, halmashauri ya manispaa ya Geita lengo likiwa ni kuongeza thamani ya maonesho ya madini yanayofanyika mwezi Septemba kila mwaka.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema awamu ya kwanza yanajengwa mabanda tisa ambapo mkandarasi anatakiwa akabidhi mradi huo kabla ya Septemba 10 mwaka huu.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela
Mafundi wakiendelea na shughuli mbalimbali za ujenzi wa mabanda. Picha na Edga Rwenduru

Mhandisi Joseph Jonathan ni msimamizi wa ujenzi wa mabanda hayo anasema wanatarajia kukabidhi mradi huo kabla ya Septemba 10 mwaka huu kama ilivyopangwa.

Sauti ya Mhandisi Joseph Jonathan
Msimamizi wa ujenzi wa mabanda Mhandisi Joseph Jonathan akizungumza . Picha na Edga Rwenduru

Aidha Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wananchi kuchagamkia fursa za maonesho ya madini mwaka huu yanayotarajia kufanyika Septemba 18 hadi Septemba 28, mwaka huu.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela
Muonekano wa bango la mbele katika viwanja vya maonesho mjini Geita. Picha na Edga Rwenduru