Storm FM
Storm FM
4 September 2025, 10:19 am

Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Geita kimezindua rasmi kampeni za kunadi ilani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Na: Edga Rwenduru
Uzinduzi wa kampeni hizo umefanyika Septemba 02, mwaka huu Katika kata ya Uyovu wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo majimbo 7 kati ya 9 na kata 92 kati ya kata 122 mkoani Geita vyama vya upinzani havijasimamisha wagombea katika maeneo hayo hivyo wagombea wa CCM wanasubiri kupigiwa kura za ndiyo na hapana.
Akizungumza katika uzinduzi huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila amesema chama chao kinaingia kwenye kampeni na mtaji wa wagombea wenye uadilifu, uaminifu na wachapakazi.

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu waziri mkuu Doto Biteko amewataka watanzania kujitokeza kusikiliza sera za wagombea huku akiwasihi wagombea kutumia majukwaa ya kampeni kunadi ilani za vyama vyao na sio kutumia kampeini kueneza chuki miongoni mwa wananchi.
Mgombea wa Ubunge jimbo la Geita mjini Chacha Wambura na mgombea ubunge Jimbo la Geita Joseph Msukuma wamewaomba watanzania kuwachagua viongozi wanaotokana na chama hicho.
Awali Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM koa wa Geita Bi. Alexandarina Katabi alisema wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura mkoani Geita ni 1,532,408 huku wanachama wa CCM wakiwa ni zaidi ya laki tano hivyo wanamtaji wa kutosha wa wapiga kura.
