Storm FM
Storm FM
3 September 2025, 9:56 am

Ikumbukwe Mwenge wa uhuru ulipokelewa mkoani Geita Septemba mosi, 2025 ukitokea mkoani Mwanza ambapo umeendelea kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Na: Kale Chongela
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Grace Kigalame ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba
Makabidhiano yamefanyika asubuhi ya leo Septemba 03, 2025 katika viwanja vya shule ya msingi Wavu katika kata ya Shabaka.
Mhe. Kigalame baadaya kuupokea Mwenge wa uhuru ametoa taarifa kuwa mwenge wa Uhuru ukiwa katika wilaya ya Nyang’hwale utakimbizwa kwa kilomita 58 na kutembelea jumla ya miradi 11 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu Ismail Ally Ussi amewataka wasimamizi wa miradi na wakuu wa idara kuhakikisha taarifa zote za mradi husika zinakuwepo kwenye mradi .