Storm FM

Geita kuupokea Mwenge wa Uhuru Jumatatu

30 August 2025, 6:22 pm

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza na waandishi wa habari . Picha na Kale Chongela

Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Geita utatembelea , kukagua , kuzindua kuweka mawe ya msingi jumla ya miradi 61ya maendeleo.

Na Kale Chongela:

Mkoa wa Geita unatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru  kwa mwaka 2025 katika kijiji cha Lwezera Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita ukitokea mkoani Mwanza Septemba 01,2025.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza na waandishi wa Habari juu ya ujio wa mwenge huo katika viwanja vya Dkt Samia Suluhu Hassan mjini Geita leo Agosti 30,2025 amesema ukiwa mkoani Geita utatembelea , kukagua , kuzindua kuweka mawe ya msingi jumla ya miradi 61ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi  za kitanzania Bilioni 164.

Waandishi wa habari mkoa wa Geita wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa. Picha na Kale Chongela

Aidha ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wote wa mkoa wa Geita kushiriki kwa hali na mali katika mapokezi ya mwenge wa uhuru kwa kila maeneo ambapo utapita kwani utatembelea halmashauri zote  sita za Mkoa wa Geita.

Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu  2025 inasema jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 kwa amani na utulivu.