Storm FM
Storm FM
20 August 2025, 9:00 pm

Jamii imetakiwa kuendelea kuwakumbuka wajane kwakuwa wengi wao wanapitia changamoto nyingi hususani za kiuchumi
Na Kale Chongela:
Kanisa la TAG Heri Wenye Moyo Safi Mtaa wa Nyantorotoro B Kata ya Nyankumbu Manispaa ya Geita limetoa msaada wa vyakula kwa watu wasiojiweza pamoja na wajane wanaoishi katika mtaa huo.
Akizungumza na Storm FM leo Agosti 18,2025 Mchungaji wa Kanisa hilo Eliya George amesema vyakula hivyo vimetokana na sadaka zinazotolewa na waumini pamoja na wananchi wanaounga mkono jitihada za kuendesha mikutano ya Injili za mitaa kwa mitaa.

Baadhi ya wananchi waliopokea msaada huo wamesema wametiwa moyo na kitendo hicho cha kanisa, wakieleza kuwa kimewasaidia kukabiliana na changamoto za upungufu wa chakula majumbani mwao.
Kwa upande wake, Balozi wa shina namba 20 Damiani Kagoma ameeleza kuwa msaada huo umeleta faraja kubwa katika jamii yake na kuonesha mfano wa mshikamano wa kijamii huku akisisitiza wananchi wa eneo hilo kuendeleza moyo wa kujitolea na kusaidiana.