Storm FM

TPF yawataka wananchi Geita kulinda amani

11 August 2025, 12:00 pm

Viongozi mbalimbali wa TPF Mkoa wa Geita baada ya kumaliza mkutano mkuu katika mji wa Katoro. Picha na Mrisho Sadick

Tanzania Peace Familiy (TPF) ni taasisi ya Kiraia inayofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na vyombo vya dola katika kulinda amani ya nchi.

Na Mrisho Sadick:

Wananchi Mkoani Geita wametakiwa kuilinda amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuwafichua watu wenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao kabla hawajaleta madhara.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Peace Family (TPF) Mkoa wa Geita Bw Faraji Juma kwenye mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo uliofanyika mjini wa Katoro wilayani Geita Agosti 10,2025 ambapo amesema ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha amani iliyopo inaendelea kudumu hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Viongozi wa TPF wakiwa kwenye mkutano mkuu wa mkoa wa Geita katika mji wa Katoro. Picha na Mrisho Sadick

Viongozi wa Taasisi hiyo Benjamin James , Dorikas Amos kutoka wilaya ya Chato na Felix Paul kutoka wilaya ya Bukombe wameitaka jamii kuendelea kushirikiana na serikali kuilinda amani ya nchi kwa wivu mkubwa kwakuwa hakuna taifa lingine mbadala wa Tanzania.

Kwa upande wake Mratibu wa TPF Kanda ya ziwa Nkanga Malima amesema TPF ni taasisi ya Kiraia inayofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na vyombo vya dola nakwamba jukumu la kulinda amani ya nchi ni wajibu wa kila mtanzania.

Viongozi wa TPF wakiwa kwenye mkutano mkuu wa mkoa wa Geita katika mji wa Katoro. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya ripoti kamili ya stori hii