Storm FM

Wachimbaji Geita waomba mitaala ya madini VETA

31 July 2025, 8:40 pm

Wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu Geita wakiwa katika shughuli zao. Picha na Edga Rwenduru

Maendeleo ya teknolojia yameleta mabadiliko makubwa katika sekta ya madini huku serikali ikikumbushwa kuwekeza katika ujuzi kwa vijana.

Na Edga Rwenduru:

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu mkoani Geita wameiomba Serikali kutumia Chuo cha VETA Geita kuanzisha mitaala maalum ya kuwajengea vijana ujuzi wa uchimbaji kulingana na jiografia ya mkoa huo.

Wakielezea maoni yao, wachimbaji hao wamesema hatua hiyo itasaidia kuongeza maarifa kwa vijana wanaojihusisha na shughuli za madini, na hivyo kuongeza tija na usalama katika kazi zao.

Aidha, wameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya uchimbaji, jambo ambalo wanasema limechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa uzalishaji wa madini katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita.

Wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu Geita wakiwa katika shughuli zao. Picha na Edga Rwenduru

Mmoja wa wachimbaji hao ambae ameajiri idadi kubwa ya vijana Seif Rajabu Seif, amesema maendeleo ya kiteknolojia yameleta mabadiliko makubwa katika sekta hiyo, ambapo wachimbaji wengi sasa wameachana na mbinu za jadi na badala yake wanatumia teknolojia za kisasa kuongeza ufanisi na usalama katika uchimbaji.

Sauti ya taarifa kamili ya stori hii na Edga Rwenduru