Storm FM
Storm FM
18 July 2025, 5:06 pm

Tangu kuanzishwa kwa Kili Challenge mwaka 2002 imelenga kukusanya Dola za Kimarekani Milioni Moja kila mwaka.
Na Mwandishi Wetu:
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu Mhandisi Jackson Masaka leo Julai 18,2025 ameongoza zoezi la uzinduzi wa GGM Kili Challenge 2025 katika Lango la Machame wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza katika hafla hiyo mhandisi Jackson amesema amewapongeza Jumla ya washiriki 67 walioshiriki kwa mwaka huu ikijumuisha Wapanda mlima 47 na waendesha baiskeli 17 kwa ushiriki wao kwa mwaka huu ambapo wamekabidhiwa bendera kwa ajili ya kuanza shughuli ya kupanda mlima safari inayoashiria kuanza kwa safari ya kishujaa “Paa la Afrika” kwa ajili ya kuunga mkono mapambano ya kitaifa dhidi ya VVU na UKIMWI

Akiwa katika hafla hiyo Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti wa Masuala ya Uendelevu na Mambo ya Ubia (Afrika), Simon Shayo, amesema GGM Kili Challenge ni harakati inayoonyesha nguvu ya umoja na dhamira ya kumaliza VVU/UKIMWI katika jamii nakueleza baadhi ya miradi wanayoitekeleza hasa katika mkoa wa Geita.
Amesema kuwa Fedha zitakazochangwa kupitia tukio hili zitaelekezwa moja kwa moja katika shughuli za kuzuia, kupima, kutibu, kuhudumia na kuelimisha kuhusu VVU/UKIMWI kupitia Kili Challenge Trust Fund, ikinufaisha maelfu ya Watanzania kote nchini

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Yasin Absa, amepongeza ushirikiano wa muda mrefu na GGML, na kueleza takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini na njia amabazo zinaendelea kutumika kutokomeza virusi vya ukimwi
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, Kili Challenge imelenga kukusanya Dola za Kimarekani Milioni Moja kila mwaka, na imechangia kwa kiasi kikubwa katika programu za UKIMWI zinazotegemea jamii, hasa katika maeneo ambayo ni vigumu kufikika.