Storm FM
Storm FM
16 July 2025, 5:52 pm

Oparesheni ya kusaka raia wa kigeni wanaoishi nchini kinyume na utaratibu mkoani Geita imezaa matunda
Na Kale Chongela:
Idara ya Uhamiaji Mkoani Geita katika oparesheni zake imefanikiwa kuwakamata nakuwarudisha makwao raia wa kigeni 126 waliongia nchini kinyume Cha Sheria Kutoka nchi jirani ya Burundi.
Akizungumzia Oparesheni hiyo katika Ofisi za Idara hiyo Magogo Mkoani Geita Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoani Geita James Mwanjotile amesema wahamiaji hao wamekamatwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita nakwamba hadi Juni 30,2025 Idara hiyo imefanikiwa kuwakamata nakuwapeleka makwao raia wa kigeni 593 idadi kubwa ni Kutoka Taifa la Burundi na mataifa ya Afrika Mashariki.

Mwanjotile amewataka wananchi Mkoani Geita kuendelea kushirikiana na Idara hiyo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kukabiliana na wimbi hilo.

Kwa upande wao baadhi ya raia hao wa Burundi Ndaijimana Helodi na Biziman Gerlad waliokamatwa wameeleza sababu ya kukimbilia nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na utafutaji wa maisha.