Storm FM
Storm FM
12 July 2025, 5:01 pm

Kutimuliwa kwa madereva wa mizigo eneo lao la kupaki Shilabela Manispaa ya Geita lachukua sura mpya
Na Kale Chongela:
Madereva wa magari ya mzigo yanayopaki pembezoni mwa barabara katika Mtaa wa Shilabela Kata ya Buhalahala Manispaa ya Geita Mkoani Geita wamepinga kauli ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ya kuwataka kuondoka katika eneo hilo bila sababu za msingi.
Wakizungumza na Storm FM baadhi ya madereva hao wamebainisha kuwa wamekuta kuna bango linalodaiwa kuwekwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo lakuwataka kuondoka katika eneo hilo huku wakisema hawawezi kuondoka hadi pale serikali itakapo watafutia eneo lingine kwa ajili ya kupaki magari yao.

Mlinzi wa magari hayo Bw RobartWest amesema baada ya kufika katika eneo hilo alikuta bango lenye maandishi yanayosomeka ni maarufuku kupaki magari eneo hili jambao ambalo yeye binafsi limempa wakati mgumu
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bw Fredrick Masalu amekiri kuweka bango hilo na kwamba ni kutokana na magari yanayopaki eneo hilo kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira sambamba na uwepo wa madalali wanaoingiza kipato kupitia magari hayo kwa maslahi yao binafsi.