Storm FM
Storm FM
12 July 2025, 4:43 pm

kutembea umbali mrefu , ajali za barabarani zimewasukuma wakazi wa Mji Mwema kuanzisha ujenzi wa soko la mtaa
Na Edga Rwenduru:
Wakazi wa Kitongoji cha Mji Mwema Kata ya Lulembela wilayani Mbogwe Mkoani Geita wameamua kuanzisha Ujenzi wa soko la Kitongoji hicho ili kuepukana na Changamoto ya kutembea umbali mrefu pamoja na ajali wakati wa kuvuka Barabara kuelekea soko la Lulembela kufuata huduma.
Ujenzi wa soko hilo umepitishwa kupitia mikutano halali ya Kitongoji hicho huku Wananchi wakielezea furaha hayo pindi soko hilo litakapo kamilika nakuanza kutoa huduma huku wakiiomba serikali na wadau wa maendeleo kuwashika mkono ili kukamilisha kazi hiyo kwa wkati.

Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Kitongoji hicho amesema walikubaliana kila kaya kuchangia shilingi Elfu 10,500 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo nakwamba wamenunua Ardhi yenye ukubwa wa ekari mbili kwa ajili ya soko hilo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mji Mwema Mashaka Mawengaya amesema Mapato yote yatakayopatikana katika soko hilo yatasaidia ununuzi wa chakula katika shule ya msingi Magufuli.