Storm FM

Shilabela waanzisha ujenzi wa ofisi ya mtaa

10 July 2025, 8:29 pm

Wakazi wa Shilabela wakijitolea kushirikia ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa huo. Picha na Kale Chongela

Zaidi ya miaka 25 serikali ya mtaa wa Shilabela Manispaa ya Geita imekuwa ikiishi katka ofisi za kupanga katika majumba ya watu.

Na Kale Chongela:

Wakazi wa mtaa wa Shilabela Manispaa ya Geita wameamua kuanzisha ujenzi wa ofisi ya kudumu ya mtaa huo ili kuepukana na changamoto ya kuhama hama kutokana na kupanga kwenye nyumba za watu.

Wakiwa katika ushiriki wa zoezi la ujenzi wa Ofisi hiyo baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamesema mtaa huo haujawahi kuwa na ofisi ya kudumu badala yake wamekuwa wakipanga chumba ambacho hakiendani na hadhi ya mtaa huo.

Sauti ya wakazi wa Shilabela

Wajumbe wa Serikali ya Mtaa huo wakiwa katika zoezi hilo wamewataka Wananchi wa Mtaa huo kuunga mkono juhudi za maendeleo katika mtaa huo.

Sauti ya wajumbe wa mtaa

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa huo Fredirick Masalu amesema mtaa huo una zaidi ya miaka 25 ukiwa kwenye ofisi za kupanga jambo ambalo lilikuwa linasababisha matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya kulipia pango pamoja na kuhama hama.

Sauti ya Mwenyekiti