Storm FM
Storm FM
8 July 2025, 7:15 pm

Ngozi imekuwa na matumizi mengi kama kutengeneza viatu na bidhaa nyingine lakini kwa Geita imekuwa tofauti.
Na Mrisho Sadick:
Kijana Robert Charles Mkazi wa Mwembeni Kata ya Nyankumbu Manispaa ya Geita ameamua kujishughulisha na kazi ya uuzaji wa ngozi choma kitoweo kipya ambacho kimeanza kushika kasi kwa kupendwa na idadi kubwa ya watu mjini Geita.
Ngozi imekuwa na matumizi mbalimbali pindi inapopelekwa viwandani tumeshuhudia bidhaa nyingi zinazotengenezwa kwa ngozi kama viatu,mabegi ya wakina mama au pochi za kike na kiume lakini kwa upande mwingine wa shilingi ngozi huliwa kama nyama za kawaida.
Kijana Charles (35) hapo awali kabla ya kuingia kwenye kazi hiyo alikuwa na kazi ya kuchuna Ng’ombe na Mbuzi Machinjioni ndipo akaamua kuanza shughuli ya kuuza ngozi choma na sasa ana uzoefu wa mwaka mmoja na jinsi inavyoandaliwa huwezi kutambua kuwa ni ngozi.

Shughuli hii ya kuuza ngozi choma ya mbuzi imemsaidia kuendesha familia yake na watoto wake watatu wanaosoma shule na amepanga Nyumba huku akiwa na mikakati ya kujenga makazi yake ya kudumu.
Dada wa Robert fatuma Mkasi anasema biashara hiyo inamnufaisha kaka yake huku kijana ambae ameajiriwa anasema kazi hiyo imemsaidia kujitegemea na kununua baiskeli yake na amepanga

Biashara yake huanza majira ya saa moja jioni katika barabara kuu ya Geita Mwanza huku baadhi ya wateja wake wakizungumzia utamu wa ngozi choma.