Storm FM
Storm FM
21 June 2025, 2:24 pm

Suala la upandishaji nauli holela bado ni kizungumkuti katika kituo kikuu cha mabasi ya abiria mjini Geita
Na Edga Rwenduru:
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Geita kwa kushirikiana na mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Geita wamebaini idadi kubwa ya mabasi ya abiria yanayofanya safari za Geita -Kagera kuwazidishia nauli abiria na baadhi ya mabasi kushindwa kutoa tiketi mtandao kwa abairia.
Akizungumza wakati wa Oparesheni iliyofanywa na Mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Geita kwa kushirikiana na polisi kitengo cha usalama barabarani katika stendi kuu ya Mabasi ya Abiria Kaimu Afisa mfawidhi RATRA Mkoa wa Geita Mukiya Juma Manyanga amesema waliokutwa na makosa hayo wamepigwa faini ya laki mbili na nusu.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Geita Phabiano Daniel amesema madereva wote wanaoendesha kwa mwendo kasi zaidi ya 99 wanafungiwa leseni kwa miezi mitatu.

Odasi Ngoma na Joseph Mugire ni viongozi wa Mabalozi wa usalama barabarani wamesema changamoto kubwa ambayo ipo magari mengi hayana mikanda na wahudumu wa magari hayo hawatoi tiketi mtandao kwa abiria