Storm FM
Storm FM
18 June 2025, 2:26 pm

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi limewakosha watu wengi kwakuwa litaondoa adha ya wananchi kuchelewa kutokana na kusubili vivuko
Na Mrisho Sadick:
Mawakala wa Mabasi yaendayo mikoani na maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Geita wametoa mabasi saba kwa ajili ya wananchi kwenda katika uzinduzi wa daraja la Kigongo Busisi ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.
Mwenyekiti wa kituo kikuu cha mabasi ya abira Mkoani Geita Khalid Fereji akiwa na mawakala hao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya abiria mkoani Geita wameanza kwa kutoa pongeza kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukamilisha ujenzi wa daraja hilo kwani itakuwa chachu ya kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Wamesema ufunguzi wa Daraja hilo Juni 19,2025 utakwenda kurahisisha usafiri kwa wananchi wakiwemo wagonjwa hasa wa Geita ambao wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kuchelewa kuvuka eneo la kigongo busisi ambapo.