Storm FM

Nishati safi yaokoa maisha ya wanawake Geita

4 June 2025, 5:19 pm

Mbunge wa viti maalumu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha miaka mitano. Picha na Mrisho Sadick

Matumizi ya nishati chafu ya kupikia kwa wanawake maeneo ya vijijini Mkoani Geita yalikuwa mwiba mchungu.

Na Mrisho Sadick:

Kuongezeka kwa matumizi ya Nishati safi ya kupikia maeneo ya vijijini imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mauaji ya Wanawake yaliyokuwa yakisababishwa na imani potofu kwa kuitwa wachawi kutokana na macho kuwa mekundu kwasababu ya moshi wa kuni.

Akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi Cha miaka mitano Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Geita Josephine Chagula amesema katika kukabiliana na matumizi ya Nishati chafu ya kupikia kwa wananchi hususani maeneo ya vijijini ameiunga mkono serikali kwa kutoa mitungi ya gesi zaidi 250 kwa makundi mbalimbali katika Jamii.

Mbunge chagula akizungumza na Storm FM kuelezea mafanikio yake katika kipindi cha miaka mitano. Picha na Mrisho Sadick

Katibu wa jumuiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Geita Bi Pili Lameck amesema mikoa ya kanda ya ziwa imepoteza watu wengi sana kutokana na imani hizo za kishrikina huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kampeni ya matumizi ya nishati safi ambayo imekuwa mkombozi kwa wananchi.

Sauti ya Mbunge na Katibu wa UWT

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Geita mbali nakupongeza kazi kubwa iliyofanywa na Mbunge huyu wameiomba serikali kuendelea kuongeza ruzuku kwenye mitungi ya gesi ili kila mtanzania aweze kutumia nishati safi ya kupikia.

Sauti ya wajumbe kamati ya utekelezaji wa UWT