Storm FM
Storm FM
2 June 2025, 6:45 pm

Geita watarajia mafanikio makubwa katika mashindano ya UMITASHUMTA baada ya mchujo makini uliofanyika kuwapata wachezaji mahiri.
Na Mrisho Sadick:
Jumla ya wanafunzi 126 wa shule za msingi kutoka mkoa wa Geita wamechaguliwa kuuwakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa yatakayofanyika mkoani Iringa kuanzia june 7 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi medali na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika michezo mbalimbali Afisa michezo mkoa wa Geita Bahati Rodgers amesema wanamichezo hao watakaa kambini kwa muda wa siku tano.
Afisa elimu mkoa wa Geita amesema licha ya kufanikiwa katika mashindano hayo kumekuwa na changamoto ya baadhi ya halmashauri kushindwa kuwasilisha michango yao kwa wakati hali ambayo imekuwa kikwazo.

Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Mohamed Gombati amewataka wanafunzi kwenda kuwa na nidhamu nakujituma ili warudi na ushindi.