Storm FM

Wapangaji 12 na mama mwenye nyumba wafurushwa Geita

29 May 2025, 12:48 pm

Wananchi wakiangalia vitu mbalimbali vya ndani vilivyotolewa nani ya nyumba. Picha na Kale Chongela

Mgogoro wa nyumba wapelekea mama mwenye nyumba (mke wa mwenye nyumba) pamoja na wapangaji wapatao 12 kuamriwa kuondoka katika nyumba hiyo.

Na: Kale Chongela:

Wapangaji 12 akiwemo mama mwenye nyumba aliyetambulika kwa jina la Chausiku Kileo kutoka mtaa wa 14 Kambarage, kata ya Buhalahala, halmashauri ya manispaa ya Geita wameiangukia serikali baada ya kudai Mahakama imetoa maelekezo ya watu hao kuondoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi kutokana na uwepo wa mgogoro wa kifamilia.

Tukio hilo limetoa Mei 28, 2025 katika mtaa huo ambapo wapangaji hao 12 na mama mwenye nyumba wametakiwa kuondoka mara moja huku wengine wakiwa hawajui wanakwenda wapi licha ya kuwa kodi zao bado hazijaisha ambapo mama mwenye nyumba ameiangukia serikali akiiomba msaada katika hilo.

Sauti ya mama mwenye nyumba Bi. Chausiku Kileo

Baadhi ya wapangaji wameeleza kusikitishwa na maamuzi hayo ambapo baadhi yao wakiwa wamelipa pesa ya kodi ambayo bado haijakwisha.

Sauti ya wapangaji

Mmiliki wa nyumba hiyo Bw. Mashaka Mathias amesema changamoto hiyo chanzo chake ni mgogoro wa kifamilia ambapo mahakama ilitoa siku 14 ili watu hao waondoke katika nyumba hiyo.

Sauti ya mmiliki wa nyumba
Mvutano ukiendelea ambapo wapangaji na mwenye nyumba wameamriwa kutoka. Picha na Kale Chongela

Mkaguzi msadizi wa Jeshi la Polisi Kata ya Buhalahala Merina Pastory akiwa katika nyumba hiyo amewataka wananchi kutoka eneo hilo kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Sauti ya mkaguzi msaidizi wa polisi kata ya Buhalahala