Storm FM
Storm FM
15 May 2025, 5:22 pm

‘Tunaendelea kumshikilia meneja wa kampuni inayolinda hapa ili aweze kutoa ushirikiano wa kubaini waliokuwa zamu ya usiku’ – Mwenyekiti wa mtaa
Na: Kale Chongela:
Maduka manne ya wafanyabiashara katika mtaa wa Mbugani kata ya Kalangalala, halmashauri ya manispaa ya Geita yamevunjwa na bidhaa zilizokuwemo ndani kuibiwa.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Mei 14, 2025 akizungumza Mwenyekiti wa wafanyabiashara katika eneo hilo Bw. Rwegasila Philibert amesemamajira ya saa kumi usiku ndipo alipata taarifa juu ya wizi huo ambapo alianza jitihada za kumtafuta meneja wa kampuni ambayo ilikuwa ikilinda eneo hilo.
Msimamizi wa kampuni ya Binson inayohusika na ulinzi eneo lililovunjwa James Kitulo amekiri wizi kufanyika ambapo amesema jitihada zinaendelea za kuwatafuta walinzi ambao walikuwa zamu huku akiahindi kulipa gharama zote zilizotokana na wizi huo.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mbugani Jumanne Bayasabe amemshikilia msimamizi huyo ili aweze kutoa ushirikianao ikiwemo kufahamu waliokuwa wanalinda eneo hilo.
Afisa Mtendaji wa kata ya Kalangalala Bw. Hamad Hussein amethibitisha kutokea kwa tukio na kuitaka kampuni hiyo kutenda haki ikiwemo wafanyabiashara kulipwa fidia zao.