Storm FM
Storm FM
10 May 2025, 9:17 pm

CHADEMA yaendelea na kampeni yake ya No reforms, no election katika mikoa ya kanda ya ziwa na leo mei 10,2025 ni zamu ya mkoa wa Geita.
Na Mrisho Sadick:
Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika amewataka wanachama wa chama hicho kuungana nakuondoa tofauti zao baada ya uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni ili kuendeleza mapambano ya kudai mabadiliko.
Mnyika ametoa kauli hiyo katika viwanja vya msufini Manispaa ya Geita Mkoani Geita katika muendelezo wa kampeni ya chama hicho ya No reforms, no Election kwa kuwataka wanachama wa CHADEMA kuvunja makundi ili kuendeleza mapambano ya kudai mabadiliko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Victoria Ezekiel Wenje ametangaza kutokukihama chama hicho mbele ya mkutano huo kwa madai kuwa kimebeba matumaini ya watu wengi.