Storm FM

Daniel akamatwa na nguzo ya wizi Nyantorotoro B

22 April 2025, 9:45 am

Muonekano wa moja ya nguzo ya umeme katika mtaa wa Nyantorotoro B. Picha na Kale Chongela

Licha ya serikali kutoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu mbalimbali katika maeneo yote, bado baadhi ya wananchi wanahujumu miundombinu hiyo.

Na: Kale Chongela:

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Daniel Robert mkazi wa mtaa wa Nyantorotoro A, kata ya Nyankumbu katika halmashauri ya manispaa ya Geita amekamatwa na nguzo ya umeme ya wizi katika mtaa wa Nyantorotoro B .

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyantorotoro B  Bw. Juma Seif Ally amethibitisha kukamatwa kwa kijana huyo na kueleza  kuwa amekutwa akifanya tukio la kuiba nguzo ya umeme katika mtaa huo na kufafanua kuwa mahojiano ya awali na kijana huyo amekiri na kusema kuwa hilo ni tukio la tatu la kuiba nguzo za umeme.

Sauti ya mwenyekiti

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo kwa nyakati tofauti wamebainisha kuwa ipo haja kwa kila mwananchi kushirikiana katika kulinda miundombinu ya umeme na kwamba aliyekamatwa anatakiwa kuadhibiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Sauti ya wananchi