Storm FM

Jogoo latoa funza muda mfupi baada ya kuchinjwa Nyakabale

17 April 2025, 11:42 am

Muonekano wa kuku aina ya Jogoo ikiwa imechinjwa na kukutwa na funza ndani.

‘Baada ya kuona afya yake inazorota ikabidi nimchinje na ndipo nikaona hayo maajabu sasa’ – Mmiliki wa kuku aina ya jogoo

Na: Paul William:

Katika hali isiyo ya kawaida Bi. Nusra Said mkazi wa kata ya Nyakabale katika halmashauri ya manispaa ya Geita amejikuta akipigwa butwaa mara baada ya kuchinja kuku kwa ajili ya kitoweo na kukuta funza wamejaa ndani ya kuku huyo.

Tukio hilo limetokea Aprili 12, 2025 ambapo Bi Nusra ameelezea mkasa mzima wa tukio hilo akisema alinunua kuku huyo kutoka kijiji cha nkome wilayani Geita ambapo alipofika nyumbani kwake alikutana na binti aliyemwambia amchinje kuku huyo kwani kanawiri sana.

Sauti ya Bi. Nusra Said

Bibi (jina lake tunalihifadhi) wa binti aliyemueleza Bi. Nusra kumchinja kuku hapo awali baada ya kumnunua ameshangazwa pia na tukio hilo na kueleza kuwa hajawahi kuliona tangu azaliwe.

Sauti ya bibi

Balozi wa eneo hilo Bahati Lusalo amekiri kulitambua tukio hilo baada ya kupewa taarifa na mmliki wa kuku hiyo.

Sauti ya Balozi Bahati Lusalo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM ambaye pia ni Polisi Jamii na mtemi mstaafu Yusuph Luchagula maarufu kwa jina la Malamba amesema licha ya kufanya kazi kwenye kijiji hicho hajawahi kukutana na tukio kama hilo.

Sauti ya M/Kiti Jumuiya ya wazazi CCM