Storm FM
Storm FM
14 April 2025, 1:30 pm

Kuanza kutolewa kwa mikopo ya asilimia 10 kumewaibua wananchi kudai kupatiwa elimu ya namna ya kuomba mikopo hiyo.
Na Mrisho Sadick:
Wananchi wilayani Nyangh’wale Mkoani Geita wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya mikopo ya asilimia 10 kwakuwa idadi kubwa ya wananchi hawana elimu ya kutosha juu mikopo hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa kijiji cha Kayenze Kata ya kafita wilayani Nyangh’wale kwenye mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Bi Anjela Enock amesema licha ya serikali kuwapatia mikopo ya asilimia 10 ameiomba kutoa elimu zaidi ili kuepukana na changamoto ya wananchi kushindwa kujitokeza kuomba mikopo hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyangh’wale Husna Tony amesema halmashauri hiyo imeendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana , wanawake na watu wenye ulemavu nakuahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya utaratibu wa kuomba na kurejesha mikopo hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholous Kasendamila amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha anaendelea kutoa elimu kwa wananchi huku akisema chama hicho imeaminiwa na wananchi ndio maana bado kipo madarakani.